Tuesday, June 21, 2011

SERIKALI YAPANGA KUDHIBITI BEI YA CHAKULA KWA KUUZA CHAKULA KUTOKA KWENYE HIFADHI YA TAIFA!

Serikali imepanga kudhibiti mfumuko wa bei nchini kwa kuuza sehemu ya chakula kilichokuwepo katika hifadhi ya chakula kwa bei nafuu pamoja na kukamilisha taratibu za uagizaji mafuta kwa pamoja .

Naibu waziri wa Fedha na Uchumi PEREIRA SILIMA amesema serikali inapitia upya mchanganuo wa tozo zilizopo katika bei za mafuta kwa lengo la kuzipunguza na kupunguza makali yak bei ya nisharti katika mfumuko wa bei.
Ameitaka sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika uwekezaji wa sekta za kilimo na nisharti ili kusaidia kupunguza ghalama za maisha kwa wananchi hasa wenye kipato cha chini na kukuza uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment