Wednesday, June 8, 2011

WHO YAKABIDHI MSAADA WA MAGARI MATATU KWA WIZARA YA AFYA!

Shirika la Afya Duniani (WHO), limekabidhi msaada wa Magari matatu kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa lengo la kuimarisha huduma za Afya nchini ikiwa ni pamoja na kuwezesha mpango wa taifa wa chanjo kufanikiwa.

Akipokea Msaada huo, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali watu, Dakta GILBERT MLIGA, amesema msaada huo utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza kasi ya vifo vya watoto nchini vitokanavyo na magonjwa mbalimbali yakiwemo polio, surua pamoja na pepo punda.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema Shirika hilo, limeahidi kutoa msaada wa magari mengine matatu kwa wizara hiyo kwa lengo lakuwasaidia maofisa mbalimbali Afya kuweza kufika kwa urahisi katika maeneo kadhaa hapa nchini ili kusimamia huduma za chanjo kwa watoto.

No comments:

Post a Comment