Wednesday, June 8, 2011

WIZARA YA KAZI YABUNI MPANGO WA KUELIMISHA JUU YA SHERIA ZA KAZI KWA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI!

                                  Waziri wa Kazi na Ajira, GAUDENSIA KABAKA
Wizara ya Kazi na Ajira imebuni mpango wa uelimishaji juu ya sheria za kazi kwa waajiri na wafanyakazi ili kuwaongezea mahusiano kazini na uelewa juu ya sheria, haki na wajibu wao katika utekelezaji wa majukumu yao.
Waziri wa Kazi na Ajira, GAUDENCIA KABAKA amesema mpango huo utasaidia kusimamia na kutekeleza Sheria za Kazi ambazo watumishi wa kada mbalimbali wanapaswa kuzifuata.
Mpango huo tayari umeshaanza kutekelezwa rasmi Machi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment