Wednesday, May 11, 2011

WATU TAKRIBANI 309,163 WAUGUA MALARIA MWAKA JANA!

                                                                      Mbu wa Maralia
Imeelezwa kuwa watu wapatao 309,163 wameugua ugonjwa wa Malaria kwa mwaka 2010, huku idadi ya watu 1,063 wakiwemo watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakitajwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa malaria kwa mwaka uliopita.

Hayo yamebainishwa leo katika Taarifa fupi ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza nakusomwa na Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk MESHACK MASSI.


Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakazi wa Mwanza wako katika hatari kubwa kupata malaria kutokana na kuwa katika ukanda wa mazalio ya mbu waenezao ugonjwa wa malaria kwa vile sehemu kubwa ya ardhi inatuamisha maji kwa muda mrefu, kupata mvua za vuli na masika kwa mwaka sambamba na eneo lake kubwa la ardhi kuzungukwa na mwambao wa ziwa Victoria.
Jamii imepata athari kubwa kutokana na ugonjwa wa malaria ikiwa ni pamoja na kudhoofu kwa afya ambayo ni nguvu kazi kwa watu wake ambayo imesababisha wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo na kuwa chanzo cha umasikini ikiwa ni zao la kushindwa kutekeleza majukumu ya shughuli za kila siku za maendeleo.

No comments:

Post a Comment