Thursday, June 23, 2011

VIJANA WANA NAFASI YA KUHAKIKISHA UCHUMI WA NCHI UNAKUA!

                            Mratibu wa vipindi wa CLOUDS FM, Sebastian Maganga
Imeelezwa kuwa vijana wananafasi kubwa katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakua, kupitia taaluma mbalimbali wanazozipata .

Mratibu wa vipindi wa CLOUDS FM, Sebastian Maganga ameyasema hayo wakati akikabidhi hundi ya shilingi milioni moja kwa wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani , ambao wameibuka washindi katika shindano la kutafuta mshindi ambaye ataonyesha uwezo wa kujijenga kiuchumi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa junior achievement Tanzania MARIA NGOWI amesema mashindano hayo yanapanua uwezo wa vijana ambao wengi wao wakimaliza masomo wanakabiliwa na changamoto za kujiajiri.

No comments:

Post a Comment