Tuesday, December 20, 2011

BARAZA KUU LA WAISLAMU TANZANIA BAKWATA LAPINGA MAANDAMANO YA WAHADHIRI KUPINGA MARIDHIANO YA SERIKALI NA MAKANISA!

Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), limesema kuwa haliungi mkono maandamano yaliyopangwa kufanyika Desemba 23, Mwaka huu, ambayo yaliandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Kiislam nchini kupinga maridhiano ya Serikali na Makanisa pamoja na kushinikiza uundwaji wa Mahakama ya Kadhi.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, ALHAD MUSSA SALUM, amewataka Waislam wote Jijini kutojiingiza katika maandamano hayo ambayo hayana tija yoyote zaidi ya kuvunja heshima ya dini hiyo kwani tayari madai hayo yanashughulikiwa na Masheikh mbalimbali walioteuliwa kwa jili ya zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment