Thursday, June 23, 2011

MARIE STOPS YAZINDUA MPANGO WA KUJIKINGA NA UKIMWI!

Jeshi la polisi nchini likishirikiana na asasi isiyokuwa ya serikali Marie Stopes wamezindua sera ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi sehemu ya kazi kwa kuepuka tabia hatarishi na kuwajali wanaoishi na virusi ukiwa mpango utakaolenga kutokomeza maambukizi kwa wafanyakazi na kuondoa athari zitokanazo na ugonjwa wa UKIMWI kwa askari na familia zao ili kuongeza tija na utendaji sehemu ya kazi.

Kamanda wa polisi kikosi cha Afya, ACP SERECKY MSUYA amesema uzinduzi wa sera hiyo utakuwa ni hatua ya awali katika utekelezaji wa afua za UKIMWI ili kujenga mazingira rafiki katika mapambano dhidi ya UKIMWI sehemu za kazi.
Aidha afisa Mahusiano wa MARIE STOPES, Dr. JOHNBOSCO BASO amesema kupitia elimu ya sera hiyo italiwezesha Jeshi la polisi kujikinga na maambukizi yanayotekea katika ajali za barabarani kwa kuwa na vifaa maalum vya kujikinga.

No comments:

Post a Comment