Tuesday, June 21, 2011

SERIKALI KUPANUA KINA CHA LANGO LA BANDARI HADI MITA 14!

                                                              Lango la Bandari ya Salama.
Serikali ina mkakati wakuongeza kina cha lango la bandari kutoka mita 12 hadi kufikia mita 14 na upana wa mita 240 kutoka mita 140 ili kuruhusu meli kubwa kuingia bandarini.

Naibu waziri wa uchukuzi Athuman Mfutakamba ameliambia bunge kwamba serikali inampango wakujenga gati mbili zakuhudumia kontena ili kuongeza uwezo wa bandari kuhudumia kontena zenye futi 20 kutoka 410,000 hadi milioni 1na laki2 .
Amesema kwamba serikali inajenga boa kubwa lakupakulia mafuta mchanganyiko lenye uwezo mkubwa wakuhudumia meli kubwa zenje ukubwa wa tani 120,000 ivyo kupunguza msongamano wa meli ndogo ndogo zinazoleta mafuta.

No comments:

Post a Comment