Monday, March 5, 2012

INDIA YATOA NAFASI 5 KWA MAAFISA MICHEZO KUTOKA TANZANIA KUJIFUNZA PROGRAMU ZA MICHEZO!

Kaimu balozi wa India nchini Tanzania Bi. Hemalatha Burgimath mmoja (kulia) akimkabidhi nyaraka za kusafiria Bi. Neema Msita mmoja wa maafisa michezo 5 wanaokwenda nchini India kujifunza program mbalimbali za Michezo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya ubalozi wa India jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yasoda (katikati).
Kaimu balozi wa India nchini Tanzania Bi. Hemalatha Burgimath akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Michezo na maafisa michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo mara baada ya hafla fupi ya kuwakabidhi nyaraka za kusafiria kwenda nchini India maafisa Michezo 5 kutoka mikoa mbalimbali. Picha zote na ARON MSIGWA –MAELEZO.

No comments:

Post a Comment