Tuesday, May 10, 2011

TGNP YAGUSWA NA WANAWAKE KUTOLIPIA VIFAA VYA KUJIFUNGULIA!

USSU MALYA 
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umesema umeguswa na hatua ya Serikali kuamua kulishughulikia suala la Wanawake kutotozwa fedha taslimu, ada pamoja na vifaa vya kujifungulia huku ikitarajia kuliingiza suala hilo katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2011 na 2012.


Kauli hiyo imekuja baada ya Serikali Kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutangaza kupitia vyombo mbalimbali vya Habari kuwa kuanzia mwaka wa Fedha ujao itatoa vifaa maalum vya kujifungulia kwa Wanawake wote bure bila kuwabagua.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), USU MALLYA, amesema hizo ni habari njema kwao na kwa taifa zima kwa ujumla kufuatia Wanaharakati na Wananchi kupigania haki ya Afya kwa wote , huduma nzuri na za bure kwa Wanawake wote hususani Wajawazito.

No comments:

Post a Comment