Tuesday, February 7, 2012

ZIARA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOANI MWANZA.


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

                                            TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Februari 5, 2012, amezindua Kitabu kiitwacho Uongozi na Utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika halfa fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Ndogo Mjini Mwanza.
Kitabu hicho kilichoandikwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Pius Msekwa kinaelezea uzoefu wa miaka 25 ya Mzee Msekwa katika utumishi wa umma chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu K. Nyerere.
Sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho chenye kusara 156 zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwamo mawaziri, viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Katibu Mkuu Mheshimiwa Wilson Mukama na viongozi wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza kabla ya Mheshimiwa Rais Kikwete hajazindua kitabu hicho, Mzee Msekwa amesema kuwa moja ya mambo yaliyomchochea aandike kitabu hicho ni pamoja na changamoto aliyopata kuitoa Rais Kikwete kwa viongozi wastaafu wa umma kuchangia maendelea na historia ya Tanzania kwa kuandika vitabu kuelezea uzoefu wao katika utumishi wa umma.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho, Mheshimiwa Rais Kikwete amempogeza Mzee Msekwa kwa kuandika kitabu hicho na kuwataka wastaafu wengine wa utumishi wa umma kufuata mfano wa Mzee huyo kwa kuandika uzoefu wake katika kuwatumikia Watanzania.
Kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Msekwa ameshika nafasi nyingi za madaraka katika Serikali na siasa ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu wa Bunge, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa chama cha TANU, Mtendaji Mkuu wa CCM, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu mjini Mwanza ambako leo alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Sherehe za Miaka 35 ya CCM zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Februari, 2012 

 

 MH PIUS MSEKWAakitoa machache katika sherehe za uzinduzi huo.


 Rais JAKAYA KIKWETE akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho.

 Rais JAKAYA KIKETE akiwa na MH PIUS MSEKWA katika uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment