Thursday, June 23, 2011
SHIRIKA LA NDEGE LA AIRBUS LASAINI MAKUBALIANO YA KUUZA NDEGE 180!
Shirika linalotengeneza ndege barani Ulaya la Airbus, limesema kuwa limepata maombi makubwa ya ununuzi wa ndege zake ambayo haijawahi kutokea katika historia ya biashara ya ndege.
Maombi hayo yaliletwa katika maonesho ya ndege mjini Paris, kwa kutia saini makubaliano ya kuuza ndege 180 kwa shirika la ndege la India linalosafirisha abiria kwa gharama nafuu IndiGo.
Makubaliano hayo yenye thamani ya euro bilioni 10 yanajumuisha ndege mpya 150 chapa A320 neo.
Ndege hizo A320 neo zinasemekana kutoa kiasi cha asilimia 15 pungufu katika matumizi ya mafuta ikilinganishwa na aina za zamani. Airbus inapanga kuanza kutoa ndege hizo mwishoni mwa mwaka 2015.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment