Friday, May 13, 2011

SHULE ZA SEKONDARI 15 ZA MIKOA YA PWANI, DSM NA PWANI ZAPOKEA DARUBINI 100!

Shule za Sekondari 15, kutoka Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Shinyanga zimepokea darubini mia moja kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa wasichana katika masomo ya Sayansi pamoja na kutayarisha kizazi kipya cha wataalam wa anga nchini.


Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni duniani (UNESCO) Taifa, Prof. ELIZABETH KIONDO, amesema darubini hizo zinatokana na utekelezaji wa Mpango wa Elimu ya anga kwa shule na vyuo vya walimu na kwamba vifaa hivyo vitasaidia kuandaa mtazamo mpya katika elimu ya sayansi nchini.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, ATHUMAN MHINA, amesema watahakikisha wanatumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa ili kuongeza zaidi udadisi kwa wanafunsi juu ya Elimu ya Sayansi na kwamba vitaongeza hamasa zaidi kwa wanafunzi kujifunza masomo ya Sayansi.

No comments:

Post a Comment