Monday, February 6, 2012

Vodacom yazindua kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa wa festula

 Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akisalimiana na wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa wa festula waliolazwa katiaka hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam, baada ya kuzindua kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa huo. .

 Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwaelekeza jambo wafanyakazi wenzake kuhusiana na kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa wa festula hapa nchini,kutoka kulia Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Meneja Mahusiano na habari za mtandao Matina Nkurlu na Kaimu Mkuu wa Mahusiano wa Vodacom Rukia Mtingwa.

 Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria uzinduzi wa kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa wa festula.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya MOYO,inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa wa festula hapa nchini,kulia ni Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania
Mwamvita Makamba. 

  Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya MOYO,inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa wa festula hapa nchini,kulia ni mmoja wa wanawake alietibiwa ugonjwa wa huo katika hospitali ya CCBRT Stella Nzyemba.

No comments:

Post a Comment