Sunday, February 26, 2012

VODACOM FOUNDATION YAKARABATI KITUO CHA POLISI MTO WA MBU KWA MARA YA KWANZA TANGIA KIJENGWE MWAKA 1967.



Hichi ni Kituo cha Polisi Cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kikionekana katika muonekano mpya baada ya kukarabatiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kiasi cha shilingi Milioni 17 kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Thobiasi Andengenye akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wakati wa hafla ya kukabidhiwa kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha , kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Tanzania kwa thamani ya Shilingi Milioni 17 tangia kijengwe mwaka 1967.katikati ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu ( OCD ) Mathias Nyange.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Jumla ya shilingi Milioni 17 zilitumika katika kukarabati kituo hiuchi. Kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini.Nguvu Kamando.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kushoto akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando kulia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba akishuhudia, Jumla ya shilingi Milioni17zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.
Baadhi ya wananchi wa Mto wa Mbu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wakishuhudia Makabidhiano rasmi ya Kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo mara baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 17.

No comments:

Post a Comment