NSSF YATIA SAINI MKATABA WA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI!
Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF limetiliana saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigamboni na Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group Co Ltd mradi utakaochukua miaka mitatu ambapo utekelezaji wake utagharimu zaidi ya Bilioni 214 .6 hadi kukamilika.
Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo, Waziri wa Ujenzi DK JOHN MAGUFULI amesema kukamilika kwa daraja hilo kutapunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam na kutumia fursa hiyo kumuomba mkandarasi aliyeshinda zabuni hiyo kutekeleza mradi huo kabla ya muda huo aliopangiwa.
No comments:
Post a Comment