Thursday, January 19, 2012

MINI ZIFF RED CARPET NDANI YA NEW MAISHA CLUB!

                                             Mwandaaji wa Min ZIFF-DANIEL NYALUSI

Na bloger team
WASANI nyota na maarufu wa filamu na muziki wa Bongo wanatarajia kupita kwenye zuria jekundu maalum (Red carpet) katika tafrija iliyoandaliwa maalum na Zanzibar International Film Festival (ZIFF) kupitia Min ZIFF ( Min ZIFF Red Carpet ) ndani ya ukumbi wa New Maisha Club Jumapili ya Januari 22 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari,jana jijini dare s Salaam, Meneja wa matamasha wa ZIFF, Daniel Nyalusi alisema kua taratibu zote tayari zimeshakamilika na wasanii hao kutoka Bongo movie na Bongofleva watapamba usiku huo wa ‘Min ZIFF RED CARPET’ ambao utakua ni wa aina yake na kasha kufuatia onesho maalum kutoka kwa maasimu wawili i AT na Offside Trick katika jukwaa moja.


“Kwa mara ya kwanza, ZIFF imeweza kuwakutanisha AT na Offside Trick, katika jukwaa moja si siku ya kukosa..” alisema Nyalusi.


Aidha, alisema kua, MINI ZIFF RED CARPET inaandaliwa kufungua kampeni ya “ Nunua kazi halisi ya msanii wa nyumbani ili kukuza tasnia ya sanaa nchini(Buy Original Product of our Artists to support the Development of Arts in Tanzania") . ambapo imeamua kufanya hivyo ilikusaidia kusambaza ujumbe kuwafikia watanzania wote ambao wengi wao wamekua wakinunua kazi zisizo halisi (Pirated Copies) na hivyo kuwanyima mapato wasanii ambao wamekua wakijitahidi katika kujikwamua kimaisha na kukuza tasnia nzima ya sanaa hapa nchini.


Nyalusi pia aliongeza kua, katika Red Carpet ZIFF itatoa tuzo maalum (Nishani- Medal) kwa Kampuni bora iliyotoa mchango mkubwa kwa sanaa ya filamu Tanzania kwa mwaka 2011, Muigizaji bora wa kiume kwa 2011, mwigizaji Bora wa kike kwa 2011, filamu bora kwa mwaka 2011 na muugizaji bora anayechipukia.


Aliongeza kua, baada ya hapo, MINI ZIFF itaendelea Ngome Kongwe Zanzibar, Januari 27 na 28,2012, kwa kuonyesha filamu za Kiswahili (Bongo Movies) sita katika screen kubwa ya Amphitheatre ndani ya Ngomekongwe kuanzia saa moja usiku na filamu zitakazo oneshwa ni Mr.President ya Steve Nyerere, Big Daddy ya Kanumba, Pamoja ya Pastor Myamba, Dj Ben ya J.B, na filamu mpya toka CL& CY production.


Aidha, siku ya Ijumaa Januari 27 na Jumamosi 28, filamu zitaonyeshwa bure kasha itafuatiwa na maonyesho ya mavazi kutoka kwa Lucky Creation na Mgece Makory kisha litafungwa na burudani kutoka kwa AT na Offside Trick kwa kiingilio cha shilingi 3,000” limalizia Nyalusi.

No comments:

Post a Comment