Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wametoa maoni yao kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara na kubainisha kwamba kudumaa kwa sekta ya Elimu nchini ni changamoto inayolikabili taifa katika kupata wataalam bora.
Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wamesema, ingawa taifa limepata maendeleo katika miundombinu ya barabara, sekta ya elimu imedumaa, kwani kiwango cha elimu kinachotolewa hakiendani na mahitaji halisi ya ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Ifikapo saa sita usiku, Watanzania kote nchini wataungana kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambayo itaambatana na matukio mbalimbali ya mkesha, ya maadhimisho hayo itakayofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja, Mbagala Zakhem na Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment