Thursday, December 8, 2011

SERIKALI YAKUSANYA BILIONI 823.7 KUTOKA SEKTA YA MIGODI KWA KIPINDI CHA MIAKA 12!

Serikali imesema katika kipindi cha miaka 12 , imevuna takribani shilingi bilioni 823.62 kutoka kwa wamiliki wa migodi mikubwa ya dhahabu nchini.

Waziri wa nishati na madini WILLIAM NGELEJA amesema katika kuhakikisha makampuni yanayochimba madini nchini yanalipa kodi inayostahili tayari kampuni ya African Barrick Gold imekubali kuanza kulipa mrahaba kwa kiwango cha asilimia nne ya mauzo halisi ya dhahabu.


Amesema mazungumzo yanaendelea na makampuni ya Anglogold Ashanti na Resolute Tanzania Limited, ili waweze kulipa asilimia nne ya mrahaba.

No comments:

Post a Comment