Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NHIF), Emmanuel Humba (wa pili kulia) na viongozi wengine wa mfuko huo,wakionesha katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, tuzo mbalimbali ikiwemo ya ushindi wa jumla Afrika (aliyoishika) iliyotolewa kwa NHIF na Taasisi ya Kimataifa ya Mashirika ya Hifadhi ya Jamii (ISSA), jijini Arusha hivi karibuni.Kutoka kushoto ni Meneja Masoko na Elimu kwa Umma, Anjela Mziray, Mkuu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Rehan Athuman na Mkurugenzi Uendeshaji, Eugen Mikongoti.

Na Mwandishi Wetu
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF), umekabidhiwa tuzo ya heshima na Taasisi ya Kimataifa ya Mashirika ya Hifadhi ya Jamii ( ISSA) ikiwa ni baada ya kuibuka Mshindi wa Kwanza wa jumla Barani Afrika kwa taasisi na mashirika yanayotoa huduma hiyo kwa mwaka 2008 na 2011.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. EMANUEL HUMBA amesema baadhi ya mambo yaliyochangia kupata tuzo hiyo ni pamoja na jinsi Mfuko huo unavyoongeza Wanachama wake na kupeleka kusogeza huduma zake mikoa mbalimbali nchini.
Dkt. HUMBA ameongeza kuwa Mfuko huo umeadhimia kuweka vituo vyake kila mkoa nchini kwa lengo la kuwasogezea huduma hiyo Wanachama wake.
No comments:
Post a Comment