Spika wa Bunge ANNE MAKINDA amekiri kuongezwa kwa posho za wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kubainisha kuwa ongezeko hilo limepitishwa na vikao halali kwa kuzingatia hali halisi ya kupanda kwa gharama za maisha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Spika MAKINDA amesema, anashangazwa na upotoshwaji unaofanywa kuhusu posho hizo kwa kutajwa kwa viwango vikubwa kuliko vilivyoongezwa kutoka shilingi elfu sabini hadi shilingi 200,000 na kwamba wanaolipwa ni wabunge wanaohudhuria kikao kwa siku husika.
SPIKA wa Bunge pia ametetea kiwango cha mishahara wanacholipwa wabunge kuwa ni kidogo, ikilinganishwa na majukumu waliyonayo katika kuwatumikia wananchi wanaowawakilisha bungeni..
No comments:
Post a Comment