Wednesday, December 7, 2011

AIRTEL MONEY YAZINDULIWA ILI KUFIKISHA HUDUMA ZA KIBENKI VIJIJINI!


Mgeni rasmi,Waziri wa fedha na Uchumi,Mh Mustafa Mkulo pamoja na Mkurugenzi wa Airtel Money Kelvin Twisa wakizindua huduma ya Airtel Money kutoka Airtel Tanzania, hafla hiyo imefanyika kwenye hotel ya Hyatt-Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw.Sam Elangallor akishuhudia tukio hilo.

Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua upya huduma ya pesa mkononi iitwayo Airtel Money itakayowawezesha wateja wa Airtel kufaidika na huduma za kibenki ambazo ni nafuu, salama na zenye uhakika zaidi kwa kupitia simu zao za mkononi.


Kiwango na ubora wa huduma vitatoa fursa kwa wateja na jamii kwa ujumla kufaidika na kukua kwa teknolojia kwa kuweza kufanya mihamala mbalimbali kwa urahisi zaidi kupitia simu ya mkononi ya Airtel.

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuzindua huduma ya Airtel Money, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sam Elangalloor alisema” Huduma ya kibenki Kwa njia ya simu za mkononi itasaidia sana kuboresha maedeleo ya jamii kwa kiwango kikubwa ikiwa tu mpangilio na ubunifu wa bidhaa umezingatia sana maeneo muhimu ya jamii kama tulivyofanya kupitia Airtel Money.


“Ujio Mpya wa huduma ya Airtel money itawezesha wateja kufanya baadhi ya malipo yakibenki kupitia simu zao kama vile kulipa Ankara za huduma mbalimabli, kuongeza muda wa maongezi pamoja na kutuma au kupokea pesa” alisema Bw Sam.


“Wakazi wengi wa vijijini wamekuwa wakikosa huduma kama hizi za kibenki kutokana kushindwa kumudu gharama inayotokana na umbali wa kufata huduma hizo mbali na vjiji vijiji vyao, lakini kwa kupitia huduma ya Airtel Money wateja wote wenye maeneo ya mjini na vijijini sasa wataweza kupata huduma za kifedha nafuu na za kisasa kwa kutumia mtandao wa Airtel ulioenea nchini kote .


Mtandao mpana tulionao Airtel katika maeneo ya vijijini unaenda sambamba na kuwa na Wakala wengi watakaotoa huduma ya Airtel Money ili kuendelea kuunganisha maeneo muhimu yatakayofaidisha watumiaji na kutoa huduma za kisasa zaidi ikiwa ni pamoja na kuunganisha ulipaji wa Ankara mbalimbali za mashirika na taasisi muhimu zinazoendana na mfumo huu wa kibenki kupitia mtandao


Kwa upande wake waziri wa fedha na uchumi, Mh Mustafa Mkulo aliwapongeza Airtel Tanzania kwa kushirikiana na serikali katika kupenyeza huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi ili kusaidia kuinua uchumi. Alisema nimefarijika sana kuona huduma za simu zinafanya baadhi ya huduma zilizo sambamba na zile za benki.

Hii ni moja ya mikakati ya kuendeleza huduma za kibenki ambayo serikali yetu ilijiwekea miaka miwili iliyopita Aliongeza” kwa kupitia mtandao wa Airtel ulioenea zaidi hasa vijijini kutawezesha idadi kubwa ya wakazi wa vijijini kujikita kwenye shughuli za biashara wakati ambapo tunaendelea kufikia malengo tuliojiwekea katika hadi ifikapo mwaka 2025.

Tunaamini Airtel money itakuwa chachu ya kusaidia shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, madini, uvuvi na matokeo yake kwa jumla ni kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi yetu.


Naye waziri wa Sayansi na Teknologia Mh. Makame Mbarawa aliongeza “Ni dhahiri kabisa kukua kwa sekta ya mawasiliano katika nchi yetu yameleta chachu kwa maendeleo ya wakulima,wavuvi, wachimba madini na wafanyabiashara mbalimbali kuweza kuwasiliana na kufanya shughuli za uzalishaji kwa ufanisi Zaidi.

Taasisi za kifedha na kibenki yanaweza kua hayajawafikia watanzania kwa kiasi kikubwa.Changamoto kwao sasa ni kuweza kufanya kazi kwa pamoja kama washirika katika maendeleo na makampuni ya simu kupitia huduma mbalimbali kama Airtel money ili kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi na
hatimaye kusaidia watanzania kwa ujumla.


Sisi kama wizara tunaahidi kushirikiana na makampuni mbalimbali ya simu ikiwemo Airtel pamoja na mitandao kwa ujumla kuhakikisha Tanzania inakua moja kati ya nchi inayotoa huduma madhubuti na za kisasa Zaidi.


Kwa Upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha Airtel Money Bw. Kelvin Twissa alisema “ huduma ya Airtel Money itapatikana kwa wateja wote wa malipo ya kabla na baada na kujiunga na huduma hii ni bure katika vituo vyetu vyote vya Airtel na mawakala wote walioenea nchi nzima.


Wakala wa Airtel Money waliosambaa nchi nzima watawawezesha wateja kufanya miamala ya pesa popote walipo. Mara mteja atakapoweka pesa kwenye akaunti yake ya Airtel Money ataweza kutuma hela, kununua muda wa maongezi au kulipia ankara za mahitaji mbalimbali ya kila siku wakati wowote au kufanya manunuzi bila usumbufu kwa urahisi mahali popote nchini.


Airtel tumejipanga kuhakikisha tunafikia malengo ya Milenia ya kuondoa umasikini na kuongeza Mapato ya taifa ya ndani kwa ujumla (GDP) kwa kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali kama kilimo na huduma za fedha zikiwepo taasisi ndogondogo za fedha, Ushirikiano wetu uliopo tangu awali kati yetu na shirika la tumbaku katika kusimamia taarifa za msimu mbalimbali kwa wakulima sasa tutaliunganisha na hili la huduma za kibenki kupitia Simu ya mkononi kusaidia kuongeza tija zaidi kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania” alisema Twissa.

No comments:

Post a Comment