Monday, December 5, 2011

MUSSA HUSSEIN WA 'USWAZI' AIBUKA TENA NA KUTAJA MKAKATI WAKE UTAKAOMTOA MAFICHONI!

*AZUNGUMZA NA KUWEKA WAZI MIKAKATI YAKE IJAYO.
* ASHAURI ABIRIA KUFAHAMISHWA MBINU ZA KUJIOKOA

SWALI: Nini kitakuwa tofauti na vipindi vingine vya TV ambavyo umewahi kufanya.?

MUSSA HUSSEIN: Kitu ambacho kitakuwa tofauti na show nyingine ambazo mimi nimewahi kufanya ni kwamba hapa nitakupa stori za ajali za kuzama kwa meli sio ya Nungwi pekee bali hata zilizopita nikikuonyesha matukio yenyewe yalivyokuwa tofauti na unaposoma kwenye gazeti au kusikia redioni. Kwa mfano katika taarifa ya habari utaonyeshwa kwa sekunde 30 tu mchezo umekwisha. Hivyo huwezi kugundua haya matukio ni makubwa au ni madogo kiasi gani.
SWALI: Nini kimekufanya ufikie maamuzi ya kufanya kipindi cha namna hii kinachoonyesha matukio halisi au huridhishwi na jinsi taarifa za majanga zinavyotolewa?

MUSSA HUSSEIN: Kwanza watanzania hatuna utamaduni wa kusoma, ila ninachoshukuru Mungu kwa sasa hivi kuna ongezeko kubwa la watanzania wanaotazama TV au mitandao hii mingine iliyopo, kwa kutokea hapo nikaona kwa sababu kila siku tunatoa lawama kwa serikali wakati mwingine tunalaumiana wenyewe kwa wenyewe ipo haja ya kupeana elimu wenyewe kuhusiana na majanga yanayotokea kila mara ikiwemo kwenye maji, barabarani au popote pale.


Kwa sababu kila siku anayeandika anasema Ajali za Barabarani zitatumaliza, Ajali za angani zitatumaliza, Ajali za majini zitatumaliza kila siku ni hivyo hivyo. Na ukiangalia hizi ajali za sijui meli, treni, mabasi zinaua mamia ya watu.

No comments:

Post a Comment