Wakati huohuo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA imesema mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha athari kubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam zinatarajiwa kuendelea hadi Desemba 23 mwaka huu kutokana na kuongezeka kwa hali ya joto la Bahari ya Hindi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo AGNES KIJAZI amesema sambamba na joto hilo kuna msukumo wa hewa yenye unyevunyevu kutoka misitu ya Congo na kusababisha makutano ya upepo mkali eneo la Mashariki na Kusini Magharibi mwa nchi.
No comments:
Post a Comment