Sunday, November 13, 2011

VODACOM TANZANIA YATANGAZA ZAWADI KWA WASHINDI WA TIKISA!


Meneja huduma na Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Elihuruma Ngowi akionyesha Tablet V9 moja ya zawadi ya zitakazotolewa kwa washindi wawili wa kwanza katika fainali za shindano la TIKISA litakalofanyika mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Vodacom (kushoto) ni Meneja wa Power House Ndg. Octavian Francis.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Vodacom Najenjwa Mbaga (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa washiriki wa fainali za TIKISA kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kitengo hicho kwa wateja wake pindi walipopata fursa ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania (kulia kwake) ni Meneja wa huduma kwa wateja Bi. Edith Ezekiel.
Washiriki wa fainali za shindano la TIKISA wakipata maelekezo kutoka kwa Mtoa huduma kwa wateja wa Vodacom Bw. Nemes Kimati jinsi wanavyohudumia wateja wao pindi walipotembelea Ofisi za Vodacom Tanzania ikiwa ni safari yao kuelekea katika kilele cha shindano hilo mwishoni wa wiki.

No comments:

Post a Comment