Sunday, October 16, 2011

VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA WATAJWA KURUDISHA NYUMA JUHUDI ZA MABARAZA YA WATOTO!

Baadhi ya viongozi wa Serikali za Mitaa nchini wametajwa kurudisha nyuma juhudi za Mabaraza ya Watoto katika kukabiliana na vitendo vya kikatili dhidi yao kwa kutowapa ushirikiano pindi wanaporipoti kwao vitendo hivyo.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa kujadili Mradi wa Haki kwa wengi wasio kuwa na Sauti, Jijini Dar es salaam lililoandaliwa na Shirika la kimataifa la SAVE THE CHILDREN, Mwakilishi wa Mabaraza ya Watoto, IDRISA MCHOLA, amesema viongozi hao pia wamekuwa wakijimilikisha vifaa mbalimbali ambavyo hutolewa kwaajili ya Mabaraza hayo hatua inayokwamisha utekelezaji wa majukumu yao.


Mwakilishi huyo ameongeza kuwa kuna haja kwa Viongozi na Wazazi nchini kushirikiana na Mabaraza ya Watoto katika kukabiliana na watu wanaokiuka haki za Watoto.

No comments:

Post a Comment