Wazazi nchini wametakiwa kuwaruhusu watoto wao kujiunga na SCOUT ili kuwawezesha kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo ya kujikinga na majanga na kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ikiwemo kuendeleza usafi wa mazingira.
Akizungumza katika mafunzo ya mawasiliano kwa njia ya Hewa yanayojulikana kama JAMBOLII ya hewani kwa kutumia Kompyuta na AMACHA Radio kwa SCOUT Afisa elimu ya watu wazima Manispaa ya Ilala Bi. ANGELINA MAJINGE amesema SCOUT wamekuwa msaada mkubwa kwa Taifa pindi yanapotokea maafa.
Naye Kamishna wa SCOUT mkoa wa Dar es Salaam ABUBAKARI MTITU amesema kwa muda wa siku tatu SCOUT duniani kote wanafanya mawasiliano kwa njia ya hewa kuhusiana na Amani, Mazingira na kupashana habari kuhusiana na majanga ya asili.
No comments:
Post a Comment