Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera amewataka waandishi wa habari za michezo kuacha dhana potofu ya kuripoti habari za uchochezi na badala yake waripoti zile habari zinazoelimisha jamii kwa ujumla.
Bendera alitoa kauli hiyo wakati wa semina ya waandishi wa habari za michezo waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mkuu huyo alisema kumekuwa na huruka ya waandishi wengi kupenda kuripoti habari za migogoro jambo ambalo linachochea migogoro na kupelekea kushusha taaluma ya michezo hapa nchini. Hali kadhalika hali hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego ambaye alifunga mafunzo hayo yaliyoshirikisha jumla ya waandishi 40 kutoka mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam, chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano Vodacom Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wakati akifunga mafunzo hayo alisema waandishi wa michezo pia wanatakiwa kuacha ushabiki wa Simba na Yanga kitendo ambacho kinachangia kupotosha sekta nzima ya uandishi wa habari za michezo. ‘’Nawaomba mzingatie mafunzo mliopata ili kuboresha zaidi sekta ya habari za michezo,” alisema Dendego.
Alisema TASWA imefanya jambo la muhimu kuandaa mafunzo hayo kitendo ambacho kimetoa changamoto kwa wanahabari kuripoti habari znye usahihi tofauti na vyo saa wmekuwa wakiripoti habari za ushabkzaidi
Aliongeza kusema si kila siku mnaegemea kuandika migogoro na habari ambazo hazina tija kwa jamii ya wanamichezo wa Tanzania mnatakiwa kuandika habari ya uhakika kutokana na kwamba waandishi ni kioo cha jamii..
Baadhi ya waandishi wa habari za michezo wakiwa katika semina ya kuwanoa waandishi wa habari za michezo iliyoandaliwa na Taswa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Mjini Morogoro.
Ameahidi pia, kushirikiana na TASWA bega kwa bega katika kuendeleza michezo nchini, kwa sababu kuna mingine kama Mpira wavu na netiboli imedorora. Kwa upande wa Vodacom kupitia Meneja Uhusiano na habari za Mtandao, Matina Nkurlu alisema, kutokana na kampuni hiyo, kwa muda mrefu imekuwa mdau muhimu katika kuendeleza sekta ya michezo Kitaifa na Kimataifa nchini haikusita kudhamini mafunzo hayo.
‘’Vodacom imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali, kama Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Vodacom Miss Tanzania, Mwanza Cycle Challenge , Kilimanjaro Marathon na Mashindano ya mbio za mashua za Vodacom Regata, imekuwa ikidhamini pia mafunzo ya kunoa waandishi wa habari kama ilivyofanya, alisema Matina.
Aliongeza kuwa: ‘’Pamoja na kufanya biashara bado tunaona ni muhimu kutoa mchango katika hii ili kuiwezesha Tanzania siku moja kuwa moja ya nchi zinazofanya vizuri kwenye michezo kama tunavyosikia majina ya nchji za Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na nyingine.’’
No comments:
Post a Comment