Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani limesema limeweka mikakati kuhakikisha matukio ya utekaji wa magari unaofanywa na majambazi kwa kutega magogo barabarani linadhibitiwa kwa kufanya doria.
Akizungumza na kituo hiki kamanda wa polisi mkoa wa pwani ERNEST MANGU amefafanua kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo kwa sasa wamejipanga vilivyo katika suala la doria hivyo ana imani kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa matukio kama hayo ya utekaji na uporaji kupungua kwa kiasi kikubwa.
Novemba 18 mwaka huu, majambazi walitegesha magogo katika eneo la mazizi lililipo eneo la kati ya lugoba na msata na kuteka magari mawili kupora mali mbali mbali, ambapo kamanda Mangu amesema tayari watu watatu wamekamatwa kuusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment