Tetemeko la ardhi lililokuwa katika kipimo cha 7.2 limelikumba eneo la mashariki ya Uturuki, na kuuwa zaidi ya watu 200. Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki amesema mapema leo asubuhi kuwa watu 239 wamethibitishwa kuwa wamefariki, na 1,090 wamejeruhiwa.
Waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan ametembelea mji ulioathirika wa Ercis ukiwa na idadi ya wakaazi wapatao 75,000 karibu na mpaka na Iran. Maafisa wamesema kuwa mamia ya watu bado hawajulikani waliko, na vikosi vya waokoaji vinaendelea kuwatafuta watu walionusurika ambao bado wako chini ya vifusi.
No comments:
Post a Comment