Wednesday, September 21, 2011

WAZIRI MSTAAFU SUMAYE AIOMBA SERIKALI KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA VYANZO MBADALA!

Waziri Mkuu Mstaafu FREDRICK SUMAYE ameiomba Serikali kutumia vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme badala ya kuendelea kutegemea vya kawaida kwa kisingizio cha kukwepa gharama za uzalishaji.

Akifafanua Mheshimiwa SUMAYE amesema jijini Dar es Salaam kuwa serikali inapaswa kutambua jukumu lake katika kuwapatia wananchi umeme ili kuepuka hasara inayopatikana ikiwemo ya kukosa wawekezaji ambayo tayari imeanza kujitokeza.


Waziri Mkuu Mstaafu SUMAYE alikuwa mmoja ya washiriki wa mdahalo wa Miundombinu ya Nishati na Madini ulioandaliwa na mfuko wa sekta binafsi TPSF ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru.
Bwawa la Mtera.

No comments:

Post a Comment