Monday, November 14, 2011

ZIARA YA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA CPC CHA CHINA!

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama Cha Kikomunisti cha China Liu Yunshan (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Chama hicho na Ujumbe wa CCM baada ya kuwa na mazungumzo, Ikulu mjini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama Cha Kikomunisti cha China Liu Yunshan baada ya mazungunzo yao Ikulu mjini Dar es Salaam, jana. Walioko nyuma, kutoka kiushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa (wapili kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama (kulia) na wengine ni Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Martine shigella, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, Katibu wa NEC, Mambo ya Nje Januari Makamba na Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, akimpa zawadi Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa baada ya mazungumzo ya ujumbe wa Chama hicho na Ujumbe wa CCM katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho na Mwenyeji wake Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM baada ya mazungumzo ya ujumbe wake na wa CCM kuwa na mazungumzo katika ukumbi wa sekretarieti, Ofisi Ndogo yab Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumumba Dar es Salaam. Wengine ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape NNauye, Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Katibu wa NEC, Uhusiano wa Kimataifa Januari Makamba.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, akiweka shada la maua kwenye eneo la Makaburi ya wataalam wa Kichina alipokwenda kuyaona, eneo la Majohe, Gongo la Mboto, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment