Tuesday, September 6, 2011

WANAFUNZI WA DARASA LA SABA KUANZA MITIHANI YAO KESHO!

Wanafunzi wa darasa la saba wanaofanya mtihani wa darasa la saba kuanzia kesho, wameshauriwa kutoingia darasani na majibu ya mitihani, ili kuepuka hatari ya kufutiwa matokeo yao.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Manyoni Magharibi, JOHN LWANJI, wakati akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mlongojii, wilaya ya Manyoni, mkoani Singida


Amesema, kitendo cha kujihusisha na karatasi zenye majibu na kuingia nazo kwenye chumba cha mtihani, kitawatia kwenye matatizo, ikiwemo uwezekano wa kufutiwa matokeo ya mtihani husika na hata kushikiliwa na vyombo vya dola.


Mheshimiwa LWANJI huyo amewataka wanafunzi hao wawe makini, waaminifu na waangalifu siku ya mtihani kuanzia kesho, pia waondoe woga, hofu na wasiwasi, ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.


Aidha, ameahidi kushughulikia matatizo mbalimbali yanayoikabili shule hiyo, likiwemo tatizo la muda mrefu la kutokuwa na mwalimu wa kike, kwa ajili ya kuwasaidia wasichana.

No comments:

Post a Comment