Akina mama wanaoishi na wafanyakazi wa kazi za ndani nchini wameombwa kuishi na wasichana hao kama watoto wao wa kuwazaa ikiwemo kuwaendeleza kielimu kutokana na mchango mkubwa wanaoutoa kwenye familia zao.
Akitoa kisa mkasa cha maisha yake, mmoja ya wasichana wanaofanya kazi za ndani kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya KIWOHEDE kwenye tamasha la kumi la jinsia linaloratibiwa na Mtandao wa Jinsia nchini TGNP amesema vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya wanawake majumbani ni kinyume na sheria.
Mbali na hayo alimshukuru mlezi wake wa sasa kwa kumuendeleza na kumsomesha fani ya ufundi ambapo kwa sasa ana ujuzi wa kupamba, kushona, kuoka na kutengeneza batiki.
No comments:
Post a Comment