Thursday, September 15, 2011

IBARA YA KATIBA NAMBA 22/23 YAPINGANA NA HAKI YA AJIRA KWA MTANZANIA ANAYEISHI PEMBEZONI!

Licha ya Ibara ya 22 na 23 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanisha kwamba ni haki ya kila Mtanzania kufanya kazi na kupata mshahara mzuri wananchi wengi hususani wanawake walio pembezoni hawajaajiriwa wala kupewa elimu juu ya haki hiyo ya kisheria.

Akitoa mada kwenye tamasha la kumi la jinsia linaloratibiwa na Mtandao wa Jinsia nchini TGNP Mwanasheria kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA, ANNAMARIE MAVENJINA amesema katika ya sasa haitekelezi ibara hiyo na kuwaacha wanawake kuendelea kuwa kundi tegemezi.


Katika hatua nyingine Mwanasheria ANNAMARIE alitoa wito kwa watunga sera kuzingatia suala hilo katika mchakato wa katiba mpya ili jamii hususani wanawake waweze kunufaika na rasilimali za nchi zao.

No comments:

Post a Comment