Monday, September 26, 2011

POLISI PWANI YAFANIKIWA KUWATIA MBARONI WAHAMIAJI HARAMU 55 WAKIWEMO 8 KUTOKA SOMALIA!

JESHI la Polisi Mkoani Pwani limefanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu 55 kati yao 8 kutoka Somalia na wengine 47 kutoka Ethiopia walioshushwa katika pori la kijiji cha Funta huko Msata wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani

Kwa mujibu wa Afisa habari wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani Athuman Mtasha amesema kuwa wahamiaji hao wamekamatwa baada ya askari waliokuwa doria kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema juu ya kuwepo kwa wahamiaji haramu hao katika pori hilo.


Bwana Mtasha amesema wahamiaji haramu hao walishushwa usiku na gari lisilofahamika na kuachwa baada ya kukosa wenyeji wa kuwapokea na dareva wa gari lililokuwa limewabeba alitoweka kwa kuhofia kukamatwa.


Aidha amesema watu hao baada ya kuhojiwa wote wamekiri kukimbia nchi zao na kuingia nchini kinyume na sheria ikiwa njia yao kuelekea Afrika ya kusini kutafuta ajira ambapo wenzao wengi wako huko wakiwa na maisha yasiyo mazuri hivyo kuja Tanzania kutafuta ajira.


Watuhumiwa hao wote 55 wanatarajia kufikishwa mahakamani katika mahakamaya hakimu mkazi kibaha kujibu tuhuma zao.

No comments:

Post a Comment