Monday, August 8, 2011

RAIS MWINYI ATAKA WAZAZI KUWASIMAMIA VIJANA WAO ILI WAFUATE MAADILI YA KITANZANIA!

Rais Mstaafu wa awamu ya pili ALHAJI ALI HASSAN MWINYI amewaomba wazazi nchini kuwasimamia vijana wao juu ya kufuata maadili mema yanayoendana na jamii ili kuwaepusha kukumbwa na suala la utandawazi na tamaduni za kimagharibi.

Alhaji MWINYI ameyasema hayo katika tafrija ya kuwakabidhi zawadi washindi waliofanya vizuri katika shindano la kuhifadhi QUR’AN kwa watoto wadogo lililofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya vijana wamekuwa wakijihusisha na matendo yasiyoendana na maadili ya Kitanzania na kuyaficha kwa kutumia mwamvuli wa utandawazi jambo linalotishia kutoweka kwa mila na desturi za Mtanzania.

No comments:

Post a Comment