Friday, August 5, 2011

SERIKALI YAIONGEZEA BILIONI 95 BAJETI YA WIZARA YA UCHUKUZI!

Serikali imeongeza fedha za Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa shilingi Bilioni 95/- ili iweze kuendana na mapendekezo yalitolewa na wabunge ya kutoipitisha bajeti hiyo hadi serikali itakapoongeza fedha zitakazotumika kuboresha miundombinu ya viwanja nya ndege, usafiri wa ndege na majini.

Akizungumza kabla ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema katika kikao chake serikali imeongeza fedha hizo zitazotumika kwenye maeneo ya reli yak kati, Shirika la Ndege ATCL na usafri wa majini ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika.


Kuhusiana na ufisadi ulijitokeza ndani ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA Mheshimiwa Pinda anasema…..


Kwa upande wa madai ya shilingi Bilioni 22/- ya malipo ya pensheni na mafao kwa wastaafu wa Shirika la Reli TAZARA Kwa upande wa Tanzania Waziri Mkuu PINDA anafafanua.

No comments:

Post a Comment