Friday, August 5, 2011

VIONGOZI KUKOSA UZALENDO CHACHU KWA TAIFA KUZOROTA KIUCHUMI!

                                JAMES LEMBELI (Kulia) akiwa na Waziri Mkuu PINDA.
Kitendo cha viongozi kukosa uzalendo wa kulitumikia taifa kimetajwa kuwa chachu ya nchi kuzorota kiuchumi na kutosimamiwa ipasavyo miradi ya maendeleo inayopangwa na serikali.

Kabla ya kukataa kuunga mkono hoja ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi iliyowasilishwa bungeni jana Mbunge wa Kahama (CCM) JAMES LEMBELI amesema licha ya wananchi kupata kero mbalimbali wao hawajali na kufurahia hali hiyo.


Katika hatua nyingine Mheshimiwa LEMBELI ameiomba serikali kuwachukulia hatua wote watakaobainika kufilisi mali za umma tofauti na sasa ambapo sheria zimekuwa zikiwalenga zaidi wananchi wanyonge.

No comments:

Post a Comment