Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Mafunzo ya wakufunzi watakaofundisha watumishi watakaoshiriki zoezi la Sensa ya Majaribio ya Watu na Makaazi yameanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa EDEMA Mjini Morogoro tayari kwa sensa hiyo itakayofanyika Septemba 4 mwaka huu.
Madhumuni ya Sensa ya Majaribio ni kupima na kutathmini maandalizi ya sensa ya mwaka 2012 inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2012.
Mafunzo hayo yatakayokuwa ya siku sita yatazingatia kupima kama madodoso yatakayotumika katika sensa ya mwaka 2012 yanakidhi malengo na matarajio na pia kuutathmini mfumo mzima wa uendeshaji wa sensa hiyo.
No comments:
Post a Comment