Thursday, August 18, 2011

KINONDONI YATENGA BILIONI 5.7 KUBORESHA MIUNDOMBINU!

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetenga jumla ya shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara na huduma za afya ambapo kwa kuanzia imepanga kuvifanya vituo vyote vya afya wilayani humo kuwa hospitali kwa lengo la kuiletea jamii maendeleo.

Akizungumza na kituo hiki Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni SEBASTIAN MHOWERA amesema bila huduma bora za afya wananchi hawawezi kujiletea maendeleo na hivyo kila jimbo litakuwa na Hospitali ya Wilaya na ile ya Mwananyamala itageuka na kuwa ya rufaa.


Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ni moja ya Wilaya iliyokuwa ikilalamikiwa na wananchi baada ya baadhi ya watendaji wake kutowajibika ipasavyo katika kutoa huduma bora kwa jamii hususani sekta za afya, elimu pamoja na miundombinu.

No comments:

Post a Comment