Thursday, August 18, 2011

CHADEMA SHINYANGA YAJIPANGA KUNYAKUA MAJIMBO YOTE UCHAGUZI 2015!

Chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mkoani Shinyanga kimesema kinaandaa mikakati ya kuhakikisha kuwa kinanyakua majimbo kata zote kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Katibu wa Chama hicho Nyangaki Shilungushela amebainisha hayo wakati wa Semina ya madiwani na kuongeza kwamba kwa wakati huu Chadema imejipanga vyema kuhakikisha inayatwaa majimbo yote ya mkoa huo.


Katika hatua nyingine Katibu huyo amewaasa madiwani wa mkoa huo kutofumbia macho masuala ya ubadhirifu wa mali za umma kwa kusimamia bajeti ya Halmashauri ipasavyo.

No comments:

Post a Comment