Meya wa Jiji la DSM Dakta DIDAS MASABURI ameitaka Bodi ya Usimamizi na Uendeshaji wa soko la Machinga Complex kufanya maamuzi magumu ya kuondoa nyaya zote zinazotumika kama vizimba kwa ajili ya kuwapangisha wafanyabiashara ili kuwepo kwa eneo zuri na bora la biashara.
Akizungumza katika majumuisho ya ziara aliyoifanya katika soko hilo, Meya wa jiji la Dar es salaam amebaini kuwepo kwa mkanganyiko wa wafanyabiashara waliopangishwa katika vizimba hivyo kwa kuilalamikia bodi kugawa mikataba kwa upendeleo.
Aidha wafanyabiashara hao wanaelezea adha wanayoipata kutokana na vizimba hivyo kuwa finyu hali inayopelekea kushindwa kuwajibika ipasavyo na kuhofia mali zao.
No comments:
Post a Comment