Trafiki akiwa kazini
Moja ya ajali za Barabarani ambapo mara nyingine kusababisha wahusika kufanya vurugu
Trafiki akimsaidia mmoja ya wazee kuvuka barabara kwa usalama
Jeshi la Polisi nchini limeombwa kuwapa askari wa usalama barabarani silaha ili kusaidia kudhibiti matukio ya uhalifu yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.
Wakizungumza na kituo hiki mara baada ya polisi kulazimika kutumia risasi za moto kuwatuliza wananchi waliopandwa na hasira baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari kumi eneo la Sayansi jijini DSM wananchi hao wamesema kama trafiki wangekuwa na silaha wangeweza kuzuia maafa zaidi yasitokee.
Ajali hiyo inadaiwa kutokea baada mtu mmoja aliyekuwa akiendesha gari aina ya Land Cruiser Prado kutaka kukimbia baada ya kumjeruhi dreva wa pikipiki wakati akitokea barabara ya Garden kuelekea barabara ya Alli Hassan Mwinyi.
No comments:
Post a Comment