Friday, July 29, 2011
WAZIRI MKUU PINDA ATOLEA UFAFANUZI UZIO WA JANGWANI JIJINI DSM!
Ofisi ya Waziri imesema imeomba kibali kutoka Ofisi ya Rais ili kupendekeza matumizi sahihi ya Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya Rais JAKAYA KIKWETE kumwagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Prof ANNA TIBAIJUKA kuvunja uzio uliojengwa katika eneo la viwanja hivyo.
Akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni Mheshimiwa IDD AZZAN wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema baada ya uchunguzi ofisi yake ilibaini kwamba uzio ule uliwekwa na mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa kituo cha mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Kuhusiana na Swali la Mbunge wa Vunjo (TLP) AUGUSTINO LYATONGA MREMA aliyetaka kujua idadi ya Vyama vya Siasa vilivyopokea ruzuku ya serikali na hesabu zake kukaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Waziri Mkuu anasema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment