Friday, July 29, 2011

VITENDO VYA UTOVU WA NIDHAMU VYAKITHIRI BUNGENI!

Vitendo vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wabunge vimeendelea kulitawala Bunge la Kumi, Mkutano wa Nne na kusababisha Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa JOB NDUGAI kuwatoa nje wabunge watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) TUNDU LISSU (Singida Mashariki), GODBLESS LEMA (Arusha) Mchungaji PETER MSIGWA Iringa Mjini kwa kikiuka kanuni.

Uamuzi huo wa Naibu Spika ulifuatia tafrani iliyojitokeza kati ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI na wabunge hao wakati waziri LUKUVI akiomba muongozo wa Spika kuhusu hotuba inayodaiwa kuwa ya uchochezi iliyosomwa na Mheshimiwa LEMA.


Tusikie muongozo wa Spika aliouomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI kuhusiana na hoja yake dhidi ya LEMA.


Akiwasilisha Bajeti ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa LEMA amesema.

No comments:

Post a Comment