Kamati kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi CCM chini ya Uenyekiti wa wa Rais JAKAYA KIKWETE imekutana leo mjini Dodoma katika kikao ambacho kinaendelea wakati wabunge wa mkutano huo wakijadili mpango kazi na utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kujaza nafasi zilizo wazi ndani yak jumuia zake.
Sambamba na hatua hizo pia Kamati Kuu itapokea na kujadili taarifa na utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yak Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kupitia kikao chake ilichokaa Aprili mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu kilichoanza leo Julai 31, 2011 katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akiingia katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma, leo Julai 31, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama.
Mwenyekiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Aman Abeid Karume (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa (kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama, wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu kilichofunguliwa leo Julai 31, katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
No comments:
Post a Comment