Friday, July 29, 2011

SERIKALI YAOMBWA KUWAONGEZEA MOTISHA ASKARI POLISI

Serikali imeombwa kuwapa motisha askari polisi kote nchini ili kupunguza vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kufanya na baadhi ya askari hao katika maeneo mbalimbali hususani ya mipaka.

Akichangia Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi) FELIX MKOSAMALI amesema vitendo vya rushwa miongoni mwa Polisi vinakithiri kutokana malipo madogo wanaopewa askari hao.


Katika hatua nyingine alitoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuweka bayana mipaka yake ili kuondoa sintofahamu miongoni mwa wananchi hususani wale wa Mkoa wa Kigoma kunakodaiwa moja ya mpaka wan chi jirani kuingia ndani ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment