Serikali imekiri kuwepo kwa baadhi ya askari polisi ambao wamekuwa wakifanyakazi bila kufuata maadili ya kazi hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Balozi Khamis Kagasheki amesema kuwa kufuatia hali hiyo wale wanaobainika wamekuwa wakichukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi.
Kauli hiyo ya Kagasheki ni kufuatia swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Rombo kupitia Chadema Joseph Selasini aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuanzisha ukaguzi wa kuwatambua baadhi ya askali polisi ambao mwenendo wao siyo mzuri.
No comments:
Post a Comment