Tuesday, June 14, 2011
WATAALAM 60 WAKUTANA KIBAHA KUJADILI ATHARI ZA UKIMWI NCHINI!
Wataalam 60 kutoka mikoa yote nchini wamekutana mjini Kibaha kujadili masuala muhimu yatakayoondoa matatizo yanayorudisha nyuma jitihada za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi hapa nchini.
Sanjari na hatua hiyo pia wataalam hao watakuwa na Fursa ya kufanya mapitio ya sheria ya Tume ya Taifa ya Ukimwi TACAIDS ya mwaka 2001 ili kuifanya iendane na hali halisi ya sasa.
Akizungumza na kituo hiki Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa TACAIDS Dakta JEROME KAMWELA amesema changamoto za uhaba wa Fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukimwi pamoja na usimamizi dhaifu wa rasilimali katika maradhi hayo ni miongoni mwa ajenda muhimu zitakazojadiliwa.
Mkutano huo unafanyika huku kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo ikiongezeka kila mwaka lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2007 unaonesha kiwango cha maambukizi kimefikia asilimia 5.8 ikilinganishwa na asilimia 7 ya mwaka 2004.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment